Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Wednesday, May 16, 2012

@HILI NALO LAHITAJI KEKI NA MASHADA YA MAUWA ??? ATC YAPATA NDEGE MBADALA.

Yapo mambo ambayo hata unapotaka kuyakalia kimya tu inakuwa shida kidogo.Jana,Shirika La Ndege Tanzania(ATC) limepata ndege mbadala(nasema mbadala badala ya mpya kwa makusudi).Ndege hii imekodishwa.Uwezo wa kununua bado hatuna.Ukikodisha kitu maana yake kiasi fulani cha iliyokuwa iwe faida yako,inakwenda kwingine. Kimsingi tunakuwa tumejikomboa kidogo sana.
Pamoja na hayo,kwetu sisi yaelekea kuwa na ndege ya kukodisha ni mafanikio makubwa sana.Yanastahili makofi,vigelegele na keki.Kweli??
Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakishuka katika ndegempya aina ya Boeing 737-500 iliyokodishwa na shirika hilo yenye uwezo wa kubeba abiria 108. Ndege hiyo itaanza kuruka baada ya wiki moja.
Kaimu Mkurugenzi na Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Paul Chizi akiongea na waandishi wa habari mara bada ya kuwasili kwa ndege mpya aina ya Boeing 737-500 iliyokodishwa na shirika hilo yenye uwezo wa kubeba abiria 108.
Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakikata keki kusherekea ujio wa ndege ndege mpya aina ya Boeing 737-500. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi na Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL ) Paul Chizi

Picha na maelezo ya picha kwa hisani ya G.Sengo

READ MORE ON http://www.bongocelebrity.com/

1 comment:

  1. hii naipinga kwa herufi ikubwa, ukute ndege yenyewe ni used

    ReplyDelete