Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, May 11, 2012

KAKA PIUS WAIKUMBUKA HII -Koffi Olomide - Inch allah

kofii olomide naweza sema ni miongoni mwa wanamuziki ambao walinivutia na kunifanya kuupenda sana muziki wa africa hasa huu wa dance, kutokana na uwezo wake na ushawishi mkubwa alionao pindi aimbapo au tuseme katika tungo zake ni mwanamuziki pekee alienisababisha mimi sophia kusema yes Muziki wa Afrika sasa unakuja kwa mabadiliko,sababu nyingine pia ni  pale alipochukua vijana kama kina Fally ipupa, Gispon, Ferre gola,lola mwana, monatana kamenga, kina suzuki, kina soleil wanga, na wengineo wengi amao kwa mawazo yao na uelewa wao wa kizazi kipya cha 4 wakaubadili muziki na kuufanya kuwa wa kisasa zaidi , mie naamini kabisa kuwa baada ya kofii olomide kufanya mabadiliko katika muziki , nazungumzia kuanzia uimbaji ushirikishwaji wa vijana na hata mavazi utoaji wa video nzuri hakika muziki wa dance ulianza kubadilika kwa kasi




Ndio maana leo tunaona vijana hao wanaojiita wa kizazi kipya cha 5 hiki cha kina fally ipupa na kina ferre Gola sasa wakiwa na nguvu ya kusimama na kumiliki bandi kwa kuwa walijifunza kutoka kwa wakongwe kama kina kofii, kina papa wemba na wengine wengi.
 leo nimeamka ijumaa hii nikajikuta nauimba huu wimbo wa inshalah video ya kwanza hapo juu ni miongoni mwa nyimbo kali za mwanamuziki Kofii olomide ambazo naamini hazitakufa kamwe au kupotea kabisa katika ulimwengu wa muziki ni tamu sana nyingine ya pili ni Hii hapa chini zifuatilie kwa makini.

Naomba uburudike  nazo zote  kisha mwisho hebu tujadili jambao.







JE KOFFI OLOMIDE UNADHANI ATAENDELEA KUTAMBA KAMA ALIVYOTAMBA ENZI HIZO WAKATI AKIWA NA KUNDI LA
QUARTIER LATIN INTERNATIONALE, JE UNADHANI KOFII ANAWEZA KUTISHA KAMA ALIVYOWAHI KUTISHA NA KUNDI HILO HAPO MWANZONI !?? LAKINI JE???? MATUMAINI YA MUZIKI WA DANCE AFRIKA NI YAPI . IJUMAA NJEMA WADAU

No comments:

Post a Comment