Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Wednesday, May 2, 2012

Space Shuttle Discovery + mazungumzo Ya MUBELWA BANDIO na DR THOMAS. HEBU FUATILIA MENGI MAZURI NDANI YAKE.

Picha ya maktaba ikionyesha Space Shuttle Discovery ikiwa kwenye Launch Pad tayari kwa safari ya kwenda kwenye space station.
Leo hii, Space Shuttle Discovery imesafirishwa kuja hapa Washington DC ambako itawekwa kwenye jumba la makumbusho ya kiTaifa ya Ndege na Anga la Steven F. Udvar-Hazy lililopo katibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Washington Dulles.
Space shuttle Discovery ikiwa "mgongoni" mwa ndege maalum ya Boeing 747 ambayo hutumika kusubiri kusafirishwa kuja Virginia Space Shuttle Discovery ikianza safari kuelekea VirginiaSpace Shuttle Discovery ikiwa imebebwa juu ya ndege ya Boeing 747 ikizunguka National Mall kwa ajili ya wananchi kushuhudia
Space Shuttle Discovery ikiwa imebebwa juu ya ndege ya Boeing 747 ikizunguka juu ya uwanja wa ndege wa Reagan kwa ajili ya wananchi kushuhudia
Photo Credits:The National Air and Space Museum and NASA
Kwa mujibu wa NASA, Space Shuttle Discovery ina heshima kubwa zaidi kuliko nyingine kutokana na sifa mbalimbali iliwamo
1:
Kuwa Space shuttle iliyofanya kazi kwa muda mrefu zaidi. Ikumbukwe space shuttle ya kwanza kufanya kazi ilikuwa Columbua ambayo ililipuka ilipokuwa ikirejea kukamilisha mission yake ya 28).
2: Discovery imefanya safari 39 kati ya mwaka 1984 - 2011 na imetumia siku 365 kwenye orbit.
3: Jumla ya wanasayansi 246 wametumia shuttle hii.
4: Ilitumika kama shuttle ya uokozi / m'badala baada ya ajali za Space shuttle Challenger na Columbia.
5: Ilikuwa shuttle ya kwanza kuwa chini ya Kamanda mwenye asili ya kiAfrika Frederick Gregory kwama 1989 na pia marubani wanawake Eileen Collins (1995)na Pamela Melroy (2000)
6: Ndiyo iliyokamilisha safari ya 100 ya space shuttle mwaka 2000
Nikimhoji Dr Donald Thomas Jumanne, Nov 29, 2011Mwishoni mwa mwaka jana nilipata nafasi ya kuzungumza na Dr Donald Thomas. Mkurugenzi katika Chuo Kikuu cha Towson hapa Maryland na ambaye amefanya kazi na NASA kwa miaka 20.
Ili mchukua miaka 33 kutimiza ndoto yake ya kwenda kwenye space, na safari yake ya kwanza aliifanya akiwa na miaka 39. Miaka 3 baadae, alikwishaenda angani mara nne na kufanya mizunguko zaidi ya 700 ya dunia.
Anaeleza mambo mengi kuanzia mwendo kasi wa shuttle (ambao ni maili 5 kwa sekunde) na namna wanavyoishi huko angani.
Pia, Dr Thomas (katika safari zake nne) alitumia space shuttle Columbia (mara tatu) na Discovery (mara moja). Hapa pia ataeleza namna ambavyo alipokea habari za mlipuko ulioharibu Columbia na kuua watu wote saba waliokuwemo ndani.
Karibu usikilize mahojiano haya

Karibu usikilize mahojiano haya
HABARI PICHA NA SAUTI KW A HISANI YA http://changamotoyetu.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment